Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 08:05

Omar al-Bashir ateuliwa kugombea nafasi ya urais 2020


Rais Omar AL-Bashir

Chama kinacho tawala nchini Sudan kimemteua Rais Omar al-Bashir kuwa mgombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.

Bashir, ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30, aliwahi kusema siku za nyuma kuwa angeachia madaraka ifikapo mwaka 2020, na alikuwa hajaweka wazi dhamiri yake ya kugombania tena.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema kwa kuwa katiba ya Sudan inaruhusu mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja, Bashir ataweza kugombea tu baada ya kubadilisha katiba.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la AFP, Bashir aliteuliwa katika mkutano wa chama madarakani uliofanyika mjiini Khartoum Alhamisi na kuendelea hadi majira ya usiku.

Rais Bashir amekuwa akiiongoza Sudan tangu mwaka 1989 baada ya kuchukua madaraka katika mageuzi ya kijeshi na ameshiriki mara mbili kwenye uchaguzi wa kinyang'anyiro tangu katiba mpya kupasishwa mwaka 2010. Bashir alishinda uchaguzi wa mwaka 2010 na 2015.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG