Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:02

Olimpiki 2020 : Mwanariadha Uchimura apoteza ubingwa


Kohei Uchimura alipokuwa akishiriki katika mashindano yanayoendelea 2020 Summer Olympics, Jumamosi, Julai 24, 2021, Tokyo, Japan. (AP Photo/Gregory Bull)
Kohei Uchimura alipokuwa akishiriki katika mashindano yanayoendelea 2020 Summer Olympics, Jumamosi, Julai 24, 2021, Tokyo, Japan. (AP Photo/Gregory Bull)

Kohei Uchimura maarufu kwa michezo ya mazoezi ya viungo yajulikanayo kama Gymnastic kwa upande wa wanaume alianguka wakati akishindana Jumamosi.

Wakati akitafuta kujitwalia taji katika kazi yake, ghafla aliteleza na kuanguka leo Jumamosi katika michezo ya Olympic inayoendelea Tokyo – Japan.

Uchimura anajulikana kwa kushinda ubingwa wa mazoezi ya viungo kwa miaka mingi.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa akitaka kushindana tu mwaka huu lakini tukio la kuanguka linamtoa nje katika mashindano hayo.

Wakati huohuo hali ya Dhoruba inaelekea Japan ikileta tishio la kuwepo mvua kubwa na upepo mkali.

Maafisa wa olimpiki wanapanga upya shuguli kadhaa za kubadilisha ratiba ya michezo mapema kabl ya athari kutokea.

Chanzo cha Habari AFP

XS
SM
MD
LG