Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 20:08

OLA yaishutumu serikali ya Ethiopia kwa kuwashambulia


Watu wakisherehekea kurejea kwa kundi lililokuwa limepigwa marufuku na serikali la Oromo Liberation Front (OLF) huko Addis Ababa, Ethiopia. Tarehe 15 Septemba, 2018. Picha na Yonas TADESSE / AFP.

Waasi kutoka mkoa wa Oromia nchini Ethiopia siku ya Jumatano waliishutumu serikali kwa kuanzisha mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi yao, baada ya mazungumzo ya amani kati ya pande mbili kumalizika bila makubaliano.

Jeshi la Oromo Liberation (OLA) lilisema vikosi vya serikali vimeanzisha "mashambulizi kwa nguvu zote" katika maeneo kadhaa huko Oromia baada ya mashauriano kumalizika mapema mwezi huu.

Msemaji wa jeshi la OLA Odaa Tarbii alisema katika ujumbe kwa shirika la habari la AFP kwamba hatua hiyo ya kijeshi "ni kinyume na matakwa ya kutuliza hatua za kijeshi kama tulivyotarajia", ingawa hakuna sitisho rasmi wa mapigano.

"Tunaliona hili ni jaribio la kupata nguvu na kutulazimisha tukubali masharti yao, lakini wasifanye makosa kuhusu nia yetu ya dhati kwa amani kuwa ni ishara ya udhaifu," aliongeza.

Odaa alisema OLA ilifungua mlango kwa ajili ya kuendelea na mashauriano, lakini aliongeza kuwa hakuna tarehe iliyopangwa kuhusu duru nyingine ya mazungumzo.

Haikuwezekana kuthibitisha madai ya OLA na wawakilishi wa wa serikali hawakujibu maombi ya shirika la habari la AFP ya kutaka watoe maoni yao.

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na jeshi la OLA -- ambalo na Addis Ababa limelitaja kuwa kundi la kigaidi mwaka 2021 -- walianzisha mazungumzo ya amani huko Tanzania katika kisiwa cha Zanzibar mwishoni mwa mwezi Aprili.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG