Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 00:37

Ocampo: Kenya inataka kuvuruga uchunguzi wa ghasia za uchaguzi


William Ruto, (kushoto nyuma) Henry Kosgey, (katikati nyuma), na Joshua Sang, (kulia) mbele ya mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC Aprili 7, 2011

Mwendesha mkuu wa mashtaka wa ICC, anasema maafisa wa Kenya wanafanaya kampeni za kuhujumu uchunguzi wake katika ghasia na mauwaji baada ya uchaguzi wa 2007

Bw Luis Moreno-Ocampo katika taarifa aliyotowa Jumapili anasema maafisa wa Kenya wanaongoza kampeni za kisiasa na kikanda ili kusitisha kesi dhidi ya watuhumiwa sita wanaodaiwa walipanga ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2007 na 2008.

Anasema kampeni hizo zinatoa ujumbe mbaya na kuendeleza hali ya uwoga kwa kuwa inawatishia wale ambao huwenda wakawa mashahidi muhimu katika kesi hizo.

Bw Moreno-Ocampo alitoa taarifa hiyo siku mojha kabla ya kuwasili kwa ujumbe wa ICC mjini Nairobi.

takriban watu 1,300 waliuwawa na maelfu kupoteza makazi yao katika ghasia mbaya kabisa za baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya. ICC inawachunguza wanasiasa sita mashuhuri wa Kenya wanaotuhumiwa kuwa na jukumu kubwa katika ghasia hizo.

Viongozi wa Kenya walikubali kushirikiana na uchunguzi huo hapo mwaka2009, lakini hivi karibuni wameanza kupinga mamlaka ya kisheria ya ICC katika kesi hizo wakidai kwamba Kenya yenyewe inauwezo wa kuwafungulia kesi watuhumiwa wa ghasia hizo.

XS
SM
MD
LG