Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:32

Hatua ya kwanza kuifuta 'Obamacare' yachukuliwa na Republikan


Kundi dogo la waandamanaji wakiipinga 'Obamacare'. Aug. 2013.
Kundi dogo la waandamanaji wakiipinga 'Obamacare'. Aug. 2013.

Warepublikan walishinda kwa kura 51-48 katika baraza la seneti Jumatano kupitisha taratibu ambazo zinazoruhusu kuifuta programu hiyo ya afya.

Baraza la Seneti lililo na wa Republikani wengi limechukua hatua ya kwanza katika kuondoa mpango wa afya wa rais Obama.

Warepublikan wameamua kuondoa mpango huo ambao pia hujulikana kama Obama Care kama moja ya masuala yao muhimu wakati Rais mteule Donald Trump atakapochukua madaraka.

Warepublikan walishinda Kwa kura 51-48 katika baraza la seneti lililopiga kura Jumatano kupitisha taratibu ambazo zinaruhusu sera za kuiondoa programu hiyo ya afya. Warepublikan wana viti 52 kati ya 100 katika baraza la seneti.

Kiongozi wa walio wengi katika seneti, Mitch McConnel amesema "seneti imechukua tu hatua muhimu katika kuifuta Obamacare na kuwa na sera mpya ya afya kwa kupitisha azimio ambalo linatoa nyenzo ya kisheria iliyo muhimu katika kuifuta sheria hiyo iliyoshindwa wakati tukielekea mbele na kuwa na sera bora za afya."

Baraza la Wawakilishi, ambako warepublikan pia wana wajumbe wengi, linatarajiwa kupiga kuhusu azimio hili wiki hii. Viongozi wa Republikan wanapanga kuandaa rasimu ya kuifuta sheria hiyo ifikapo mwisho wa mwezi Januari.

Trump Jumatano amesema anataka juhudi zote za kuifuta na kuja na mpango mpya wa afya ziende sambamba.

Wademokrat waliipitisha sheria hiyo mwaka 2010 wakati walipokuwa wanadhibiti mabaraza yote mawili ya bunge wakati ambapo Obama akiwa madarakani.

XS
SM
MD
LG