Mkutano wa vijana viongozi kutoka barani Afrika unaojulikana kama Mandela washington Fellowship ulimalizika alhamisi katika hoteli ya Omnishoreham Washigton Dc.
Mkutano huo uliwakutanisha pamoja vijana 1000 kutoka mataifa 49 ya barani Afrika kabla ya kufika Washington vijana hawa walikwenda katika vyuo mbali mbali hapa Marekani kwa wiki 6 kupata mafunzo na kubadilishana uzoefu wa miradi na kazi mbali mbali wanazofanya.
Na baada ya hapo ndipo walikutana na rais Barack Obama katika hitimisho la mafunzo yao .
Rais Barack Obama alizungumza na vijana hao akieleza kuwa Marekani pia inajifunza kutoka barani Afrika.
Emmanuel Odama mchungaji kijana na mshiriki wa program hii kutoka nchini Uganda ndiye aliyemkaribisha rais Obama huku akisisitiza umuhimu wa vijana wa Afrika kuendelea kufanya kazi kwa bidi kwenye maeneo yao.
Rais Obama pia alimtambua mmoja wa washiriki kutoka Tanzania Geline Fuko kwa kazi anayofanya ambapo ameweza kuasaidia kuanzisha mtandao wa kituo cha taarifa za katiba, akiwa mtafiti wa masuala ya katiba anafanya kazi na kituo cha sheria na haki za biinaadamu nchini humo ambapo mtandao huo unawawezesha watanzania kuweza kupata nakala ya katiba na taarifa zake ili kuwaruhusu watanzania kupata nafasi ya kufahamu zaidi haki na wajibu wao na kuifahamu serikali yao bila malipo yoyote.
Wakati huo huo mmoja wa washiriki kutoka Tanzania Simon Titus Malugu ametunukiwa tuzo ya USADF kwa uvumbuzi wake wa mashine ya kutotoa vifaranga vya kuku.
Na mmoja wa washiriki kutoka nchini Kenya Alantei Leng’eti ambaye ni mwanaharakati wa haki za wanawake ameeleza amepata mengi katika mkutano huu na ataendelea na juhudi zake akirudi nyumbani ili kuzuia ukeketaji ambao unaanzia kwa watoto tangu wakiwa na umri wa miaka 8, ambao pia hawapewi nafasi ya kwenda shule kwasababu ya mila potofu analenga kupinga mila hizo na pia kuunga mkono mila zilzio bora hasa kudumisha utamaduni wa mmasai.