Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 16:15

Obama kuliaga taifa Jumanne usiku akiwa Chicago


Rais Barack Obama akiwa kwenye Air Force One, Septemba 2016.
Rais Barack Obama akiwa kwenye Air Force One, Septemba 2016.

Rais wa Marekani, Barack Obama atatoa hotuba yake ambayo ikulu ya White House imeielezea kama "mitzamo wa mustakbali" katika ujumbe wa kuwaaga wananchi wa Marekani.

Hotuba ya Obama itaeleza kwa ufupi mambo aliyoweza kuyakamilisha wakati wa utawala wake wa miaka minane. Pia anakusudia "kuwashawishi watu kujihusisha na kupigania demokrasia yao," mshauri wa ngazi ya juu wa ikulu, Valerie Jarrett amewaambia waandishi wa habari Jumatatu.

Hotuba hiyo ataitoa saa tatu usiku kwa saa Marekani , kwenye eneo la McCormick, kituo cha Lakefront Convention huko Chicago, mji ambako Obama alikulia.

Msemaji wa White House, Jen Psaki amesema hotuba yake itakuwa fupi kuliko ile hotuba ya hali ya kitaifa, ambayo huwa inachukua takriban dakika 63.

Donald Trump and Rais Barack Obama
Donald Trump and Rais Barack Obama

Sherehe za kuapishwa rais mteule, Donald Trump zitafanyika Januari 20, wakati ambapo atakuwa rasmi ni rais wa 45 wa Marekani.

Wasaidizi wake wamesema kuwa rais Obama anajishughulisha katika kuandika hotuba ayke ya kuwaaga wamareknai, na anaweza kuwa anairekebisha muda wote huu mpaka atakapopanda jukwaani.

Safari ya Obama kwenda Chicago imeandaliwa kuwa ndiyo ya mwisho ya kikazi nje ya Washington kama rais, na itakuwa mara ya mwisho kutumia ndege ya Air Force One.

Rais Obama akifuta machozi wakati akihutubia
Rais Obama akifuta machozi wakati akihutubia

XS
SM
MD
LG