Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 06:22

Marekani yatoa helikopta sita kwa Kenya kupambana na ugaidi


Obama alipokuwa nchini Kenya.
Obama alipokuwa nchini Kenya.

Serikali ya Marekani, imetoa helikopta sita kwa serikali ya Kenya kusaidia katika vita vya kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Mapema Ijumaa, waziri wa ulinzi wa Kenya, Raychelle Omamo, alipokea ndege sita kati ya nane ambazo zimetolewa na Marekani, kwenye hafla iliyofanyika katika uwanja wa kijeshi wa Laikipia Air base.

Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec, alisema shehena iliyotolewa na Marekani kwa Kenya Ijumaa , ndio msaada mkubwa zaidi wa usalama kuwahi kutolewa kwa nchi ya Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.

Godec amesema kuwa mazungumzo yaliyokusudia kuimarisha ushirikiano wa kiusalama kati ya mataifa hayo mawili, yalianza mwaka wa 2010. Ndege zingine mbili zinatarajiwa kutolewa mwezi mei mwaka ujao, na kufanya thamani ya usaidizi huo wa kiusalama kufikia shilingi bilioni kumi na moja.

Balozi huyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Kenya katika vita dhidi ya ugaidi.

XS
SM
MD
LG