Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:16

Obama kuruhusu wakimbizi zaidi Marekani


Rais Barack Obama, akiwa na kiongozi wa Myanmar's Aung San Suu Kyi nyumbani kwakeYangon, Myanmar mwaka wa 2014.
Rais Barack Obama, akiwa na kiongozi wa Myanmar's Aung San Suu Kyi nyumbani kwakeYangon, Myanmar mwaka wa 2014.

Rais Barack Obama ametoa mpango wa kuruhusu wakimbizi 110,000 kuingia Marekani mwaka wa 2017 ikiashiria ongezeko la wakimbizi 10,000 zaidi kuliko ilivyopangwa .

Rais Barack Obama ana mpango wa kuruhusu wakimbizi 110,000 kuingia hapa Marekani mnamo mwaka wa 2017 ikiashiria ongezeko la wakimbizi 10,000 zaidi kuliko lengo lake la awali ikiwa ni asilimia 30 zaidi kuliko mwaka huu.

Kulingana na vyombo vya habari waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametangaza malengo hayo ya kuwapatia wakimbizi makazi Marekani hapo jana wakati wa kikao cha faragha cha kamati za sheria za baraza la seneti na lile la wawakilishi.

Mara ya mwisho kwa Marekani kuweka malengo ya kuwapokea wakimbizi kuwa ya juu kama alivyoweka rais Obama ilikua wakati ni wakati wa utawala wa Rais Bill Clinton 1995 ambapo wakimbizi 112,000 waliruhusiwa kuingia nchini.

Mwaka wa 2015, Marekani iliwakaribisha wakimbizi 70,000 pekee. Kuna uwezekano kuwa Rais Obama atatangaza rasmi mpango huo wa wakimbizi kabla ya kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Matiafa utakaofanyika

XS
SM
MD
LG