Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 04:07

Obama amaliza ziara ya Kenya, aelekea Ethiopia


Kabla ya kuondoka Nairobi Obama alihutubia wakenya mjini Nairobi, Jumapili, July 26, 2015.
Kabla ya kuondoka Nairobi Obama alihutubia wakenya mjini Nairobi, Jumapili, July 26, 2015.

Rais Barack Obama wa Marekani amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Kenya na kuondoka Jumapili alasiri kuelekea Ethiopia, taifa lingine la Afrika ambalo linapokea ugeni wa kwanza wa rais aliye madarakani Marekani.

Kabla ya kuondoka Kenya Rais Obama alihutubia umati wa watu waliojazana katika uwanja wa Kasarani na kutoa wito kwa Kenya na nchi nyingine za Afrika kuzingatia misingi inayoleta maendeleo.

Rais Obama akipunga mkono baada ya kumaliza hotuba yake kwa wakenya uwanja wa Kasarani, Nairobi.
Rais Obama akipunga mkono baada ya kumaliza hotuba yake kwa wakenya uwanja wa Kasarani, Nairobi.

Wakati wa ziara yake Kenya Rais Obama alifungua kongamano la dunia la ujasiriamali, alifanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya Rais Uhuru Kenyatta. Pia alitembelea makumbusho ya August 7 - ambayo ni kumbukumbu ya shambulizi la kigaidi la mwaka 1998 katika ubalozi wa Marekani nchini Kenya na Dar es Salaam, Tanzania.

Akiwa Ethiopia Rais Obama anatazamiwa kutoa hotuba katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, tukio ambalo pia litakuwa la kwanza katika historia ya Umoja huo.

Wachambuzi wa mambo wanajiuliza je Mwenyekiti wa sasa wa AU Robert Mugabe atakuwepo katika hotuba hiyo ama la?

XS
SM
MD
LG