Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 13:13

Obama kukutana na Netanyahu huko White House


Rais Obama akiwahutubia wanachama wa kundi la AIPAC mjini Washington, Jumapili Machi, 4, 2012

Rais Obama atakutana na Waziri Mkuu wa Israel huko Washington kuzungumzia program ya nyuklia ya Iran

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa mazungumzo juu ya program ya nyuklia ya Iran, siku moja baada ya kusema angependelea kutatua suala hili kidiplomasia badala ya kutumia nguvu.

Mkutano wa Jumatatu huko White House unafanyika wakati wasi wasi unazidi duniani kutokana na mpango wa nyuklia wa Iran na uwezekano wa Israel kuishambulia nchi hiyo.

Bwana Obama aliliambia kundi lenye ushawishi linalotetea maslahi ya Israel hapa Marekani - AIPAC mjini Washington, Jumapili kwamba hivi sasa ni wakati wa kutoa nafasi kwa “shinikizo lililoongezwa kufanya kazi” na kuimarisha ushirika wa kimataifa dhidi ya Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Katika hotuba yake kwa wanachama wa kundi hilo la AIPAC, bwana Obama alisema “tayari kuna gumzo jingi la vita na Iran. Lakini pia alithibitisha tena dhamira yake ya kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia ikiwemo kutumia hatua za kijeshi.

Bwana Netanyahu alisema Jumapili aliyashukuru matamshi ya bwana Obama kwamba “hatua zote zipo mezani” na kwamba Israel lazima ijilinde yenyewe dhidi ya kitisho chochote. Kiongozi wa Israel atalihutubia kundi la AIPAC baadae Jumatatu.

XS
SM
MD
LG