Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:41

Serikali nyingi zinasumbua wanahabari na kuzima upinzani-Obama


Rais Barack Obama akihutubia mkutano wa 71 wa baraza kuu la Umoja wa mataifa Sept. 20, 2016.
Rais Barack Obama akihutubia mkutano wa 71 wa baraza kuu la Umoja wa mataifa Sept. 20, 2016.

Rais wa Marekani Barack Obama anasema dunia lazima itambue kwamba nguvu sawa za utandawazi ambazo zimewakutanisha pamoja vilevile zimeweza kufichua mstari wa utengamano.

Katika hotuba yake ya mwisho katika mkutano baraza kuu la Umoja wa Mataifa, akiwa kama Rais wa Marekani Jumanne, Rais Obama ameelezea kuvunjika kwa makubaliano ya msingi huko mashariki ya kati na kusema jamii zetu zimegubikwa na kutokuwa na uthabiti na utulivu.

Amesema tumeona serikali nyingi zikisumbua wanahabari na kuzima upinzani na zikizuia upatikanaji wa taarifa. Rais Obama alisema, makundi ya kigaidi yanatumia mitandao ya kijamii na kuwarubuni vijana, kuhatarisha jamii huru na kuchochea chuki dhidi ya wahamiaji wasio na hatia na Waislamu.

Pamoja na hayo amesema mataifa yenye nguvu yanapinga masuala waliyowekewa na sheria za kimataifa, na kumalizia kusema hali hiyo ndiyo inayo tafsiri ulimwengu wa leo.

XS
SM
MD
LG