Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:36

Obama kutoa hotuba yake kuu ya mwisho kuhusu usalama wa kitaifa


Rais Barack Obama, na mshauri wake wa usalama wa kitaifa, Tom Donilon, kwenye picha katika bustani ya ikulu mjini Washington, iliyopigwa June 5, 2013.
Rais Barack Obama, na mshauri wake wa usalama wa kitaifa, Tom Donilon, kwenye picha katika bustani ya ikulu mjini Washington, iliyopigwa June 5, 2013.

Rais Barack Obama alasiri ya Jumanne alitarajiwa kutoa hotuba yake kuu ya mwisho, juu ya usalama wa kitaifa, akiwa kama rais. White House ilisema kuwa rais Obama angesifu jinsi sera zake za kupambana na ugaidi zilivyo walinda wananchi kutokana na vitisho kadhaa vya kigaidi, katika kipindi cha miaka minane alipokua rais.

White House iliongeza kupitia taarifa, kuwa Obama, angezungumza kwenye kambi ya kijeshi ya MacDill Airforce base iliyo kusini mashriki mwa jimbo la Florida, Marekani.

Taarifa hiyo ilisema kuwa rais huyo anayeondoka, angeelezea jinsi utawala wake ulivyojenga uhusiano na serikali za nchi mbali mbali, ili kupuunguza makali ya kundi la Islamic State, na makundi mengine ya kigaidi, bila kuongeza wanajeshi wa Marekani katika nchi hizo.

XS
SM
MD
LG