Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:15

Obama kuhutubia taifa juu ya Iraq


Rais Obama atahutubia taifa Jumanne usiku kuhusu hatua ya kuondoka kwa majeshi ya mapambo ya Marekani nchini Iraq.

Rais Barack Obama wa Marekani atahutubia taifa Jumanne usiku kuhusu kuondoka kwa majeshi ya mapambano nchini Iraq na hatua ifuatayo baada ya hapo. Atahutubia taifa kutokea katika ofisi yake White House mjini Washington baada ya kutembelea wanajeshi wa Marekani huko Ft. Bliss, Texas na pia hospitali ya kijeshi ya Walter Reed mjini Washington ambako wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu.

Rais Obama anatazamiwa kuwaelezea Wamarekani kile ambacho Marekani imefanikiwa Iraq tangu 2003, na kusisitiza nia ya Marekani kuendelea kusaidia katika juhudi za kuleta uthabiti Iraq na kushukuru wanajeshi wa Marekani waliotumikia Iraq.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani inasema wanajeshi wa Marekani waliouawa Iraq ni zaidi ya 4.400 na wengine karibu elfu 32 walijeruhiwa.

Rais Obama amesisitiza kwamba bila kujali kama mtu alimwunga mkono au kumpinga rais wa zamani George W. Bush katika uamuzi wake wa kuivamia Iraq mwaka 2003, Wamarekani ni lazima wajitolee kusaidia jeshi la Marekani kuhakikisha kuwa operesheni zote za mapigano zinamalizika.

XS
SM
MD
LG