Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:45

Obama kuwasili Kenya leo jioni


Rais Barack Obama akipunga mkono kutoka Air Force One kuelekea Kenya na Ethiopia, July 23, 2015.
Rais Barack Obama akipunga mkono kutoka Air Force One kuelekea Kenya na Ethiopia, July 23, 2015.

Karibu Obama. Ndio maneno ambayo wananchi wa Kenya waliamka nayo leo asubuhi siku ambayo Rais Barack Obama anatazamiwa kuwasili hapa mjini Nairobi kwa ziara ya siku tatu.

Ndege ya Rais Obama - Air Force One - inatazamiwa kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta leo Ijumaa majira ya magharibi na kuanza msafara wa kilomita 15 kuelekea mjini Nairobi.

Barabara kuu ya Uhuru Highway inatazamiwa kutanda maelfu ya wananchi kumkaribisha kwa shangwe rais Obama ambaye anakuja Kenya kama mwana anayerejea nyumbani kwa vile marehemu baba yake ni mzaliwa wa Kenya.

Mji wenyewe wa Nairobi uko tayari kabisa, ukiwa umesafishwa na kurembeshwa kwa namna kadha. Kuanzia mapema Ijumaa asubuhi tayari msongamano wa magari ulikuwa umepungua Nairobi kati ingawa barabara nyingi bado hazijafungwa.

Baadhi ya watu wameamua kutokwenda makazini leo na wengine wanaondoka makazini mapema ili kuepuka msongamano ambao utatokea majira ya jioni.

Atakapowasili leo rais Obama hatakuwa na shughuli yoyote rasmi hadi Jumamosi atakashirikiana na mwenzake rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kufungua mkutano mkuu wa ujasiriamali ambao unahudhuria na wajumbe kutoka kote barani Afrika na duniani kwa jumla.

XS
SM
MD
LG