Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 00:06

Obama apongeza ushirikiano na Iran


Rais Barack Obama akihotubia taifa kutoka White House
Rais Barack Obama akihotubia taifa kutoka White House

Rais Rouhani amesema, ni wapenda vita pekee ndio hawajafurahia kile alichokiita ukurasa wa dhahabu katika historia ya Iran

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:20 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais Barack Obama alitowa taarifa jana, ambayo ni nadra kutolewa siku ya Jumapili kupongeza kuachiliwa huru kwa wafungwa wa Marekani na kutetea diplomasia yake na Tehran, ikiwa ni pamoja na makubaliano ya nuklia ya mwaka jana ambayo yalifikia hatua muhimu ya kihistoria hapo jumamosi.

Rais Obama alizungumza kutoka White House muda mfupi tu baada ya Marekani kuiwekea Iran vikwazo vipya kwa ajili ya kufanya jaribio la kombora la masafa marefu yenye uwezo wa kubeba bomu la nuklia.

Obama alisema, leo ni siku nzuri. Wamarekani kadhaa walokamatwa kwa njia zisizo za haki hatiomae wanarudi nyumbani.

Rais Obama alipongeza maendeleo yaliyopatikana katika mambo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa makubaliano ya nuklia na Teheran.

Obama alisema, kabla ya makubaliano Iran ilikua inaongeza kwa makini akiba yake ya uranium iliyorutubishwa, kuweza kutengeneza hadi mabomu 10 ya nuklia. Hii leo zaidi ya asili mia 98 ya akiba hiyo imesafirshwa nje ya Iran, ikiamaanisha kwamba Iran haina kitu kilichobaki kuweza kutengeneza hata bomu moja. Tumefanikiwa kupata maendeleo haya ya kihistoria kupitia diplomasia bila ya kuanzisha vita vingine huko mashariki ya kati.

Lakini si kila mtu anaesherehkea ufanisi huo. Spika wa baraza la wawakilishi mrepublican Paul Ryan amelalamika dhidi ya kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi, akisema Tehran itatumia fedha hizo kufadhili ugaidi. Ryan aliongeza kusema kwamba vikwazo vinaondolewa wiki chache tu baada ya jaribio haramu la Iran la kombora lake ya masafa marefu.

Msimamo huo ulitolewa pia mjini Jerusalem na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Netanyahu alisema, ni wazi kuanzia hivi sasa Iran itakua na uwezo mkubwa zaidi itakayoweza kutumia kwa ajili ya vitendo vya kigaidi katika kanda hiyo na dunia nzima na Israel inajipanga kukabiliana na kitisho cha aina yeyote ile.

Kinyume na matamshi hayo, ni maamshi ya furaha kutoka katika mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon.

Bw. Ban alisema,anamatumaini kwamba pande zote zitasonga mbele kutekeleza mpango kamili wa pamoja wa utekelezaji kwa nia nzuri. Huu ni wakati wa kuimarisha ushiriikiano katiuka changamoto nyingine zilizo muhimu kupitia majadiliano.

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema hakuna aliyepoteza kitu katika mkataba wa nuklia, na ni wapenda vita pekee hawajafurahi na kile alichokieleza ukurasa wa dhahabu katika historia ya Iran

Rais Obama amesisistiza kwamba vikwazo muhimu dhidi ya Iran vingali havijaondolewa na kutangaza adhabu mpya zitakazowekewa nchi hiyo.

Obama alisema, jaribio la kombora la Iran la hivi karibuni kwa mfano lilikwenda kinyume na majukumu yake ya kimataifa na matokeo yake Marekani inaiwekea vikwazo vipya kwa watu na makampuni yanayofanya kazi kuendeleza mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran.

Obama aliahidi kutakuwepo na uangalifu zaidi wakiendelea mbele.

XS
SM
MD
LG