Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:57

Obama asisitiza umuhimu wa ukabidhianaji mamlaka kwa amani


Rais wa Marekani Barack Obama atopa hotuba mjini Athens Ugiriki
Rais wa Marekani Barack Obama atopa hotuba mjini Athens Ugiriki

Rais Barack Obama amesissitiza umuhimu kukabidhiana mamlaka kwa njia ya amani, wakati akiwahutubia wananchi wa Ugiriki kuhusu demokrasia leo Jumatano.

Obama alisema siku ya Jumatano mjini Athens kuwa licha ya kukabiliana vikali wakati wa kampeni za kuwania urais, demokrasia inategemea sana kukabidhiana mamlaka kwa njia ya amani. Rais huyo amesema kuna tofauti kubwa katiu yake na rais mteule Donald Trump, lakini akaongeza kuwa demokrasia ya Marekani ni kubwa kuliko mtu binafsi.

Aliihakikishia ulaya kwamba Marekani itaendelea kuisaidia kukabilina na visa vya utovu wa usalama, licha ya wasiwasi kwamba utawala wa Donald Trump huenda ukakumbatia na kuanza kutekeleza sera za kujitenga. Jana Jumanne, Obama alisema kuwa muungano wa kijeshi wa NATO ni muhimu mno, na unasaidia katika kuendeleza ushirikiana hata wakati hiuu wa mpito katika siasa za Marekani.

XS
SM
MD
LG