Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 20:50

Obama akiwa Boston: 'Bomu haliwezi Kutushinda'


Rais Barack Obama akizungumza wakati wa misa ya imani mbali mbali mjini Boston April 18, 2013.
Rais Barack Obama akizungumza wakati wa misa ya imani mbali mbali mjini Boston April 18, 2013.
Siku tatu baada ya mabomu kulipuka katika mbio za Boston Marathon, Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama, waliungana na maafisa wa mji huo, viongozi wa kidini na mamia ya watu kuwaombea waliouawa na wale waliojeruhiwa katika milipuko ya mabomu.

Rais Obama na mkewe walikaa katika msitari wa mbele kabisa katika kabisa la Church of the Holy Cross huku viongozi wa kidini wakisalia waliouawa, waliojeruhiwa, wafanyakazi za uokozi na watu wa Boston.

Mchungaji Liz Walker wa kanisa la Roxbury Presbyterian alizungumza nguvu ya jumuiya inayokabiliwa na maovu. Kulikuwa na dua na hutuba kutoka madhehebu mbali mbali ya kikristo, Kiyahudi na viongozi wa Kiislamu.

Meya Tom Menino wa Boston aliwasifu waliouawa katika mashambulizi hayo: Mtoto wa miaka minane Martin Richard, Krystle Campbell aliyekuwa na miaka 29 na mwanafunzi wa kutoka China Lu Lingzi aliyekuwa na umri wa miaka 23.

Rais Obama alisema moyo wa watu wa Boston kuendelea na maisha kama kawaida ni sawa na kofi kali kwa wale waliofanya kitendo hicho. Obama alisema watu wa Boston "watakimbia tena" na taifa litakuwa nao katika safari ndefu ya kurejea katika maisha yao ya kawaida.
XS
SM
MD
LG