Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:40

Obama apinga kubadili mkakati wa kupambana na Isis


U.S. President Barack Obama addresses a news conference following a working session at the Group of 20 (G20) leaders summit in the Mediterranean resort city of Antalya, Turkey, Nov. 16, 2015.
U.S. President Barack Obama addresses a news conference following a working session at the Group of 20 (G20) leaders summit in the Mediterranean resort city of Antalya, Turkey, Nov. 16, 2015.

Rais Obama alisema,tuna jeshi bora zaidi duniani, na tuna viongozi wa kijeshi wazuri zaidi duniani. Nimekuwa nikikutana nao kwa miaka sasa, kujadili hatua mbalimbali, na sio maoni yangu pekee, lakini ni maoni pia ya washauri wa karibu wa kijeshi na kiraia, kwamba litakuwa kosa kupeleka wanajeshi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais Barack Obama anasema itakuwa makosa kupeleka wanajeshi wan chi kavu kwenda kupigana dhidi ya wanamgambo wa Islamic State, akipinga wito kutoka ndani nan je ya nchi yakuitaka Marekani kuchukuwa hatuwa thabiti Zaidi kufwatia mashambulizi ya kigaidi huko Paris ijuma. Kiongozi huyo alitoa matamshi hayo katika mji wa mapumziko wa Uturuki wa Antalya mwishoni mwa mkutano wa viongozi wa G20 .

Rais Barack Obama alitumia mda wake mwingi wa siku siku mbili za mkutano wa G20 kzungumza na viongozi wenzake juu ya kile cha kufanya kuhusu kundi la Islamic State ambalo limedai kuwajibika na mashambulizi ya Paris. Wakifunga mkutano, rais Obama alikitaja kundi hilo kama uso wa uwovu na kuahidi kuongeza juhudi za kupigana dhidi yake, hata hivyo Obama alipinga kupelekwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani huko.

Rais Obama alisema,tuna jeshi bora zaidi duniani, na tuna viongozi wa kijeshi wazuri zaidi duniani. Nimekuwa nikikutana nao kwa miaka sasa, kujadili hatua mbalimbali, na sio maoni yangu pekee, lakini ni maoni pia ya washauri wa karibu wa kijeshi na kiraia, kwamba litakuwa kosa kupeleka wanajeshi.

Obama anataka kuepusha kurudia kosa la vita vya Iraq.

Bw. Obama alisema,sio kwamba jeshi letu halingeweza kwenda huko Mosul au Raqqa na kuwaondowa ISIL, lakini kwa sababu tungelishuhudia marudio ya kile tulichoshuhudia awali.

Matukio ya Paris yamewasababisha viongozi wa mataifa tajiri kutozingatia Zaidi ajenda rasmi ya biashara na uchumi. Kipaumbele cha viongozi kilikuwa kujadili mikakati ya kulishinda kundi la Islamic State na kumaliza vita huko Syria.

Viongozi wa Marekani na Russia walionekeana kuweka kando tofauti zao na kuendelea na mipango ya kusitisha vita na hatimae mabadiliko ya utawala huko Syria.

Lakini mazungumzo pekee , hayatoshi kwa Ufaransa. Taifa hilo lilifanya takriban mashambulizi ya anga 20 kwenye ngome za Isalimic state huko Iraq. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius aliyehudhuria mkutano huo kwa niaba ya rais wake, alisema nyakati ngumu zinahitaji kuwepo na hatuwa ngumu.

Bw. Fabius alisema,mtu hawezi kushambuliwa vibaya, mnajuwa kile kinachofanyika huko paris bila kuchukua hatua kali.

Kulikuwa na fununu iwapo rais Obama atachukuwa uwamuzi wa dakika ya mwisho kwenda huko Ufaransa. Badala yake, alimtuma waziri wake wa masuala ya mambo ya nje John Kerry. Kiongozi wa Marekani, anaendelea na ziara ya asia kukutana na viongozi wenzake wa kanda hiyo.

XS
SM
MD
LG