Rais Barack Obama wa Marekani amewakaribisha wabunge wa Marekani kujiunga naye kwenye ziara nya kihistoria nchini Cuba inayatarajiwa kufanyika katika muda wa wiki moja.
Ingawaje ordha ya watakaoandamana naye Rais haijatolewa, mwandishi wa VOA Michael Bowman ameweza kuzungumza na maseneta kadhaa ambao wamedhibitisha kupokea mwaliko huo.