Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 14:15

Utafiti unaonyesha Obama, Hillary wanapendwa zaidi Marekani


Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama (Kushoto) na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Hillary Clinton.

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik, Hillary Clinton, bado ndiyo watu wawili wanaopendwa zaidi na Wamarekani, kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na kampuni ya Gallup.

Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha kwamba wawili hao wameendelea kushikilia taji hilo kwa miaka kumi mfululizo, licha ya kwamba umaarufu wao umepungua kwa kiasi, ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Asilimia 17 ya wale waliohojiwa walisema Obama ndiye kiongozi anayependwa sana akilinganishwa na Rais Donald Trump aliyechukua nafasi ya pili akiwa na asilimia 14.

Clinton, ambaye kwa wakati mmoja alikuwa waziri wa mambo ya nje, alimshinda mkewe Obama, Michelle. Clinton alikuwa na asilimia 9 huku Michelle akiwa na asilimia 7.

Huu ni mwaka wa 16 mfululizo kwa kura hiyo ya maoni kumwonyesha Hillary Clinton kama mwanamke anayependwa mno.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG