Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:55

Rais Barack Obama afanya kampeni na Hillary Clinton


Rais Barack Obama akikampeni na Hillary Clinton huko Charlotte, N.C., Julai 5, 2016.
Rais Barack Obama akikampeni na Hillary Clinton huko Charlotte, N.C., Julai 5, 2016.

Rais Barack Obama na waziri wake wa zamani wa mambo ya nje Hillary Clinton wameunganisha nguvu katika kampeni wakati Clinton akitafuta nafasi ya urais wa Marekani na rais huyo wa sasa akijaribu kumhakikishia kwamba sera zake zinapita urais. Obama alitoa hotuba ya hisia akieleza kwanini anaamini wamarekani wamchague Clinton kuwa rais wa 45 wa Marekani.

“Nina shauku kubwa, Hillary amenipa shauku na niko tayari kufanya kazi!aliuambia umati wa watu waliokuwa umevutiwa mno huko Charlotte ,North Carolina Jumanne.

Obama alimwelezea waziri wake wa mambo ya nje wa zamani kuwa ni mtu mwenye uelewa mkubwa , mwenye uwezo mkubwa, anayefanya kazi kwa bidi, mwenye maamuzi magumu na kiongozi anayependa kazi yake ambaye atalinda taifa kusaidia familia zinazofanya kazi na kuinua thamani na matakwa ya Marekani.

XS
SM
MD
LG