Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 06:17

Obama amzungumzia Donald Trump


Rais Barack Obama amesema kuwa baadhi ya viongozi wa kimataifa ambao amezungumza nao wameelezea kughadhabishwa na kuwepo kwa Donald Trump kama mgombea wa urais hapa Marekani mwaka huu.

Obama mwenyewe pia amemkashifu bilionea huyo. Akizungumza na wanahabari kwenye mji wa Japana wa bandari wa Ise Shima mapema leo, baada ya kongamano la viongozi wa mataifa yalioendelea ya G7 amesema kuwa dunia inamtazama kwa makini.

Trump amekua akiongoza kwenye kampeni za chama cha Republikan kutokana na matamshi yake ya kutatanisha kuhusu wahamiaji wanaozungumza kihispania na waislamu. Trump pia amegusia kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Japan na Korea Kusini na badala yake kupatia mataifa hayo silaha za nyuklia za kukabiliana na Korea Kaskazini.

XS
SM
MD
LG