Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:16

Obama kuondoa wanajeshi 10,000 nchini Afghanistan


Rais wa Marekani Barack Obama akihutubia kutoka Ikulu
Rais wa Marekani Barack Obama akihutubia kutoka Ikulu

Katika hotuba yake Jumatano Rais Obama aliwaambia watu wa Marekani mwisho wa vita umefika.


Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza mwanzo wa kumaliza vita vya miaka 10 akiamuru kuondolewa kwa wanajeshi 33,000 wa Marekani ifikapo mwishoni mwa mwaka 2012.

Katika hotuba yake Jumatano Rais Obama aliwaambia watu wa Marekani mwisho wa vita umefika.

Amesema wanajeshi 10,000 wa mwanzo wataondolewa mwishoni mwa mwaka huu.
Wanajeshi 100,000 wa Marekani wanafanya kazi Afghanistan. Vita vya Afghanistan vimepata umaarufu mdogo kwa umma wa Marekani huku mamilioni ya dola yakitumika katika vita hivyo nchini Afghanistan na Iraq katika muongo uliopita. Rais Obama alikiri kwamba umefika wakati wa kuzingatia zaidi kuijenga Marekani.

Rais amesema ifikapo mwaka 2014 taratibu za mpito nchini Afghanistan zitakuwa zimekamilika kwa watu wa nchi hiyo kuchukua majukumu ya usalama nchini mwao.

Katika hotuba yake ya dakika 13 Rais Obama aligusia kwamba kundi la al-Qaida liko katika shinikizo zaidi tangu shambulizi la kigaidi la septemba 11 na karibu litashindwa. Majeshi maalumu ya Marekani yalimuuwa kiongozi wa al- Qaida Osama bin Laden nchini Pakistan mei 2.

Naye mchambuzi wa masuala ya kisiasa hapa Marekani bwana Mobhare Matinyi aliyefuatilia hotuba ya bwana Obama alisema ilikuwa ya kisiasa zaidi.
Bwana Matinyi alisema Rais aliahidi kuondoa majeshi ya Marekani alipogombania urais na ilimbidi atimize ahadi hiyo huku akitegemea kura za wamarekani .

Bwana Mobhare pia amesema kuondoa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan kutalegeza mzigo wa deni na labda kutasaidia kuimarisha uchumi wa Marekani.

XS
SM
MD
LG