Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:20

Obama awaelekeza washauri wake namna ya kupambana na ISIS


Wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS

Rais wa Marekani Barack Obama amewaelekeza washauri wake wa usalama wa taifa kupambana na juhudi za kundi la Islamic State-IS kuingia na kupanua harakati zao ndani ya Libya na katika nchi nyingine.

Rais Obama alisisiza kwamba Marekani itaendelea kupambana na wapanga ugaidi wa ISIS katika nchi yeyote pale inapobidi. Wasiwasi wa bwana Obama kuhusiana na ushawishi wa ISIS nchini Libya ulielezewa pia na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ash Carter siku ya Alhamis.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ash Carter
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ash Carter

Kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Pentagon bwana Carter alisema wapiganaji wa kundi la Islamic State wanajaribu kujiimarisha huko Libya kwa kuunda vituo vya kutoa mafunzo wenyewe, kuwavuta wapiganaji wa kigeni na kuchangisha fedha kupitia kodi.

Bwana Carter alisema ISIS lazima isiruhusiwe kufuata mfumo ilioutumia huko nchini Irak na Syria wa kuchukua sehemu kubwa ya ardhi ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG