Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 03:08

Obama atoa hotuba ya hali ya kitaifa ya mwaka 2012.


Rais Obama akitoa hotuba ya hali ya kitaifa.

Rais Obama amewataka wabunge wa Marekani kufuata mfano wa majeshi ya Marekani na kufanya kazi pamoja na kuunda Marekani inayoongoza dunia

Rais wa Marekani Barack Obama amesema anatoa mpango wake wa uchumi ambao anasema umejengwa kuwa wa kudumu, uchumi uliojengwa kwenye kazi za uzalishaji, nishati,mbinu za kazi kwa wafanyakazi wa Marekani na kile alichokiita kujenga upya thamani ya Umarekani.

Katika hotuba yake ya hali ya kitaifa rais Obama amewataka wabunge wa Marekani kufuata mfano wa majeshi ya Marekani na kufanya kazi pamoja na kuunda Marekani inayoongoza dunia katika elimu, na kuvutia kizazi kipya cha kazi za uzalishaji na kazi zenye kipato cha juu na kudhibiti nishati yao wenyewe.

Ametoa wito kwa uchumi ambao ufanyaji kazi bora unalipa na wajibu unalipwa. Bw.Obama amesema ahadi ya Marekani ndio suala kuu la wakati wetu na kusema hakuna changamoto iliyo zaidi na ya haraka.

XS
SM
MD
LG