Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:02

Obama awahutubia Wacuba


Rais Barack Oabama
Rais Barack Oabama

Havana iko maili 90 ambazo ni sawa na kilomita 145 kutoka jimbo la Florida hapa Marekani lakini akasema ili kufika Cuba inapaswa kwenda umbali mrefu kupita vizuizi vilivyowekwa katika historia , vizuizi vya maumivu na utengano.

Rais wa Marekani Barack Obama leo ametambua kwamba kulikuwepo historia ngumu kati ya Marekani na Cuba lakini alitoa ujumbe wa amani kwa watu wa Cuba wakati akikamilisha ziara yake katika nchi hiyo ya kikomunisti.

Havana iko maili 90 ambazo ni sawa na kilomita 145 kutoka jimbo la Florida hapa Marekani lakini akasema ili kufika Cuba inapaswa kwenda umbali mrefu kupita vizuizi vilivyowekwa katika historia , vizuizi vya maumivu na utengano. Obama aliuambia mkusanyiko wa watu waliokutana huko El Gran Teatra de Havana.

Amesema tofauti zilizopo baina ya Serikali za Washington na Havana ni za kweli na zina umuhimu wake, lakini amesema pande zote mbili zinaweza kuendelea mbele kwa kubadilisha mahusiano ya kihistoria.

Obama alitangaza kwa ujasiri kwamba amekwenda huko kuzika vita baridi vya wamarekani pamoja na kupanua wigo wa urafiki na watu wa Cuba.

Obama pia ametoa mwito wa kusitishwa vikwazo vya zamani vya kiuchumi vya Marekani katika nchi ya Cuba, ambavyo amesema ni mzigo uliopitwa na wakati kwa watu wa Cuba na badala yake wakati umefika wa kuondoa vikwazo hivyo.

Lakini rais Obama pia alilazimika kuikosoa Serikali ya Cuba akisema kuwa hata kama vikwazo vitaondolewa watu wa Cuba bado hawata weza kuishi bila kuwa na mageuzi ya kidemokrasia.

Baada ya Obama kukamilisha ziara yake, idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika ilizungumza na mchambuzi wa maswala ya Kisiasa na mhadhiri wa chuo kikuu cha Le Salle nchini Marekani kuhusu ambaye alianza kwa kuelezea umuhimu wa hotuba ya rais huyo kwa wananchi wa Cuba.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:42 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG