Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:09

Obama atoa cheti chake cha kuzaliwa


Cheti za kuzaliwa cha Rais Obama mwaka 1961
Cheti za kuzaliwa cha Rais Obama mwaka 1961

Ni hatua iliyofuatia shutuma zisizokwisha kutoka kwa baadhi ya wapinzani wanaodai kuwa hakuzaliwa katika ardhi ya Marekani

Ikulu ya Marekani Jumatano imetoa hadharani cheti za kuzaliwa cha rais Barack Obama ili kumaliza ubishi unaoletwa na baadhi ya wapinzani kuwa hakuzaliwa nchini Marekani.

Cheti hicho kamili kinaonyesha kuwa Obama alizaliwa Hawaii August 4, 1961 kwa mama Mmarekani Ann Dunham Stanley na baba Mkenya Barack Hussein Obama.

Hatua hiyo imefuatia madai ya muda mrefu kutoka kwa baadhi ya wapinzani Marekani ambao wamekuwa wakidai kuwa Rais Obama kwa hakika hakuzaliwa Marekani kwa hivyo hastahili kuwa rais wa nchi au kugombea urais wa nchi hii. Mwaka 2008 Rais Obama alitoa hati ya kuzaliwa kutoka hospitali aliyozaliwa Honolulu, Hawaii lakini wapinzani wamekuwa wakidai kuona cheti kamili.

Rais Obama alitokea mbele ya waandishi wa habari Jumatano White House mjini Washington na kusema kuwa amefanya hivyo kwa sababu haoni kwa nini watu bado wanaendelea kuzungumzia swala hilo ambalo halina ubishani.

Amesema hatatumia muda zaidi kuzungumzia swala hilo.

XS
SM
MD
LG