Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 15:32

Obama atetea Marekani kuwepo Libya


Rais Barack Obama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, June 29, 2011.
Rais Barack Obama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, June 29, 2011.

Ajibu tuhuma kutoka kwa baadhi ya wabunge kwamba anakiuka madaraka ya kivita aliyonayo kisheria

Rais Barack Obama ametetea ushiriki wa Marekani katika operesheni za NATO nchini Libya, akisema operesheni hiyo ya kimataifa imesaidia kulinda maelfu ya raia katika nchi hiyo ya Afrika kaskazini.

Obama alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington kuwa hajakiuka Azimio la Madaraka ya Kivita, sheria ya Marekani ambayo inataka rais apate ruhusa kutoka bungeni katika muda wa siku 60 endapo majeshi ya Marekani yanahusika katika mapigano.

Alisema kiongozi wa Libya Muammar Gadhafi alikuwa anatishia kuuwa watu wake, na Marekani, kama sehemu ya ushirika wa kimataifa, ilishambulia ulinzi wa anga za Libya ili msaada wa kibinadamu uweze kufikishwa kwa wananchi wa Libya. Aliserma shinikizo linamzidi kiongozi huyo wa Libya, au kama alivyosema "kitanzi kinakaza."

Rais Obama alisema alizungumza na watu wa Marekani kuhusu Libya na kuwaarifu wajumbe wa Congress na amefanya vile alivyotakiwa kufanya. Alitoa maelezo hayo kujibu madai kutoka kwa baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa amekiuka madaraka yake kwa kuyaingiza majeshi ya Marekani vitani bila ruhusa ya bunge.

XS
SM
MD
LG