Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 16:07

Obama atembelea waathiriwa wa Mafuriko Louisiana

President Barack Obama reaches to shake hands with Louisiana Gov. John Bel Edwards, after arriving on Air Force One at Baton Rouge Metropolitan Airport in Baton Rouge, Louisiana., Aug. 23, 2016.
President Barack Obama reaches to shake hands with Louisiana Gov. John Bel Edwards, after arriving on Air Force One at Baton Rouge Metropolitan Airport in Baton Rouge, Louisiana., Aug. 23, 2016.

Rais wa marekani barack Obama alitembelea jimbo la Louisiana siku ya Jumanne ambalo limekumbwa na mafuriko ya kihistoria kwenye sehemu kubwa ya kusini mwa jimbo hilo.

Hii ni safari ya kwanza ya Obama kwenda Louisiana tangu dhoruba na mafuriko yametokea kati ya Agosti 8 na 14 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 13, na uharibifu wa nyumba zipatazo 60,000 na kuwaacha maelfu ya watu wakitafuta makazi ya muda. Zaidi ya watu 160,000 wameomba msaada wa fedha kutoka serikali kuu na mpaka sasa dola milioni 20 zimesambazwa kwenye maeneo yaliyoathirika.

Rais aliwahakikishia waathirika wa mafuriko kwamba utawala wake umeweka kipaumbele cha juu katika suala la kuokoa majanga ya kibinadamu.

XS
SM
MD
LG