Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 05:37

Obama atangaza mpango mwingine wa kuinua uchumi


Rais Barack Obama akitoa hotuba huko katika jimbo la Wisconsin
Rais Barack Obama akitoa hotuba huko katika jimbo la Wisconsin

Obama atangaza mpango mwingine wa kuinua uchumi

Vyombo vya habari Marekani vinawakariri maafisa wakisema kuwa rais Barack Obama anapanga kupendekeza nafuu ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wiki hii.

Bwana Obama anatazamiwa kutangaza mpango huo Jumatano huko Cleveland, Ohio, ambao utaruhusu biashara kutoa asilimia 100 ya gharama ya uwekezaji mpya kutoka kwenye kodi zao mpaka 2011.

Mpango huo unategemewa kugharimu zaidi ya dola bilioni 200 katika miaka miwili ijayo . Bwana Obama pia anatazamiwa kutangaza mapendekezo yatakayowezesha kupunguza kodi moja kwa moja kwa utafiti wa biashara na maendeleo.

Mapendekezo hayo yatakuwa ni juhudi ya hivi karibuni ya Obama kupambana na ongezeko la ukosefu wa kazi Marekani, wiki chache kabla ya upigaji kura wa bunge mwezi November.

Jumatatu rais alipendekeza mpango wa miaka 6 wa dola bilioni 50 ili kujenga upya barabara za nchi, reli na viwanja vya ndege wakati wa hotuba yake kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wanachama wao mjini Milwaukee, Wisconsin.

XS
SM
MD
LG