Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:31

Obama atangaza mkuu mpya wa majeshi ya Marekani


Makaburi ya Kitaifa ya Arlington, ambako wanajeshi walofariki katika vita vyote huzikwa pamoja na viongozi mashuhuri wa Marekani.
Makaburi ya Kitaifa ya Arlington, ambako wanajeshi walofariki katika vita vyote huzikwa pamoja na viongozi mashuhuri wa Marekani.

Rais Barack Obama amemteuwa Jenerali wa jeshi la nchi kavu, Martin Dempsey kuwa mwenyekiti wa baraza la wakuu wa majeshi.

Rais Obama alitangaza uteuzi huo katika White House Jumatatu siku wamarekani wanatoa heshima zao kwa wale wote walotoa mhanga maisha yao kupigania nchi hii.

Jenerali Dempsey atachukuwa nafasi ya Admirali Mike Mullen, afisa mkuu wa jeshi la majini ambae muda wake unamalizika Septemba. Uteuzi wa rais wa wakuu wa majeshi unabidi kuthibitishwa na baraza la Senet, hata hivyo inatarajiwa wapunge hawatokuwa na tatizo kuidhinisha uteuzi wa Jenerali Dempsey.

Jenerali Ray Odierno, aliyetumikia mara tatu nchini Irak, ameteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la ardhini akichukua nafasi ya Jenerali Dempsey.

Kabla ya kutangaza uteuzi huo rais Obama alihudhuria sherehe za kila mwaka za kuwakumbuka walofariki vitani katika makaburi ya kitaifa ya Arlington, nje kidogo ya Washington, na kuwashukuru mashuja walotoa mhanga maisha yao katika sehemu ya kile alichokieleza kuwa ni "mnyororo usovunjika wa uzalendo" mnamo historia kamili ya Marekani.

Sherehe za Siku ya Mashuja, Jumatatu ya mwisho ya mwezi wa Mei husherekewa kila pemba ya Marekani, na huko Afghanistan, wanajeshi wa Marekani walisita kwa muda kuwakumbuka wenzao 1 400 walouwawa tangu kuanza vita mwaka 2001.

XS
SM
MD
LG