Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:10

Obama ataka mataifa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa


Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama

Makubaliano hayo yanataka mataifa 20 ya Serikali na maofisi kufanya kazi pamoja kuhakikisha taarifa zenye uhakika kuhusu matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa yanapatikana ili kuimarisha usalama wa taifa .

Rais wa Marekani Barack Obama amesema mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio linaloendelea kukua dhidi ya usalama wa taifa na matokeo yake ni lazima yahusishwe kwenye maamuzi yanayohusiana na masuala ya usalama wa taifa , mipango na hatua za kuchukuliwa.

Obama alitia saini makubaliano ya sera mpya Alhamisi iliyopita. Makubaliano hayo yanataka mataifa 20 ya Serikali na maofisi kufanya kazi pamoja kuhakikisha taarifa zenye uhakika kuhusu matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa yanapatikana ili kuimarisha usalama wa taifa .

Hatua hiyo imekuja siku hiyo ambayo baraza la usalama la masuala ya ujajusi lilipotoa ripoti likisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kusababisha changamoto za usalma wa taifa katika kipindi cha miaka 20 ijayo ikiwemo katika operesheni za jeshi la Marekani .

Baraza pia Iimesema pia mabadiliko hayo ya hali ya hewa tayari yamesababisha matatizo ya usalama wa taifa kote duniani na yanaweza kuongezeka.

XS
SM
MD
LG