Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:08

Obama asifia uchumi wa Marekani umeimarika


Rais Barack Obama akilihutubia taifa jumanne usiku kwenye jengo la bunge la Marekani, washington DC.
Rais Barack Obama wa Marekani alitoa mwito kwa bunge kuufanya mwaka 2014 kuwa mwaka wa utekelezaji.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:49 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza jumanne usiku kwenye ukumbi wa bunge la Marekani, Rais Obama alikiambia kikao cha pamoja cha bunge na mamilioni ya wamarekani wakimtazama kwenye televisheni kwamba huu unaweza kuwa mwaka wa nafuu kwa Marekani.

Akielezea mafanikio ya kiuchumi ikiwemo kuibuka tena kwa soko la nyumba na Marekani kuishinda China kama mwekezaji namba moja bwana Obama alisema Marekani ipo kwenye nafasi nzuri kwa karne ya 21 kuliko taifa jingine lolote duniani miaka mitano baada ya matatizo makubwa ya kiuchumi tangu kudorora kwa uchumi. Lakini alisema swali ni kama maafisa wa Marekani watasaidia au kudumaza maendeleo haya.

Bwana Obama alisifia muafaka wa bajeti uliofikiwa katika bunge mwezi uliopita lakini alisema unatakiwa kuiacha serikali iwe huru kulenga juu ya ubunifu wa ajira mpya, na sio kubuni matatizo mapya.

Aliwataka wabunge kufanya kazi na yeye katika miezi ijayo ambapo wanaweza kupata mafanikio ya pamoja. Na alitoa mwito kwa kulenga juu ya fursa kwa wamarekani wote hatua ambayo kama unafanya kazi kwa bidii na kuwajibika unaweza kufanikiwa.
XS
SM
MD
LG