Rais wa Marekani Barack Obama anasema anaamini nchi iko katika hatari” ikiwa Donald Trump atashinda uchaguzi ujao.
Obama alifanya kampeni kwa ajili ya Hillary Clinton jana Jumatano huko Chapell Hill North Carolina eneo ambalo lina ushindani mkubwa ambapo wagombea wote wanataka kushinda kama mmoja wao anataka kuingia White house.
Obama anasema hakuona kama nchi itakuwa hatarini kama angeshindwa katika uchaguzi dhidi ya John McCain 2008 au Mitt Romney 2012 .
Aliwaonya wapiga kura wa North Carolina kutokuridhika na kufikiri kura yao haina umuhimu. Amesema kubaki nyumbani siku ya upigaji kura kunawasaidia wale wanaotaka kuzuia sauti zao.
Rais alikuwa akizungumza na wapiga kura weusi ambao anasema hawana mwamko sana kwasababu yeye si mgombea mwaka huu.
“Nahitaji kila mtu kufahamu kwamba kila jambo tulilofanya linategemea na mimi kuweza kupeleka tochi kwa mtu ambaye anaamini katika mambo kama yale ninayoamini mimi” Obama alisema awali katika mahijiano ya radio kwenye kipindi maarufu cha asubuhi nchini Mrekani cha "Tom Joyner Morning show".