Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:20

Obama: Wamarekani wanatarajia polisi kufanya mengi kuliko uwezo wao


Rais Obama alipokutana na wanafamilia wa waathirika wa ufyatuaji risasi hapa nchini.
Rais Obama alipokutana na wanafamilia wa waathirika wa ufyatuaji risasi hapa nchini.

Rais Barack Obama alisema kuwa Marekani ina matarajio makubwa kupita kiasi kwa polisi wake ikiwa ni pamoja na kutaka wawe jawabu kwa shida zinazoikumba jamii. Bwana Obama aliyasema hayo Alhamisi katika mkutano wa maswali na majibu uliofanyika katika ukumbi mmoja wa michezo ya kuigiza uliopo mjini Washington DC.

Mkutano huo ulijadili ongezeko la hivi karibuni la visa vilivyopelekea hali tete na matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi ambayo yamekithiri katika muhula wake kama rais.

Katika mkutano huo ambao ulirushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni za kitaifa nchini Marekani ulihudhuriwa pia na wadau wengi, ikiwa ni pamoja na waathiriwa wa makabiliano na polisi kutoka majimbo ya Texas, Minnesota, Louisiana na Missouri.

Mahala palipofanyika mkutano huo palikuwa na umuhimu mkubwa kwa sababu ni barabara hiyo hiyo nambari kumi nne ambapo Wamarekani walifanya mgomo wa kupinga mauaji ya kiongozi wa kutetea haki za binadamu, Martin Luther King, alipouawa mnamo mwaka wa 1968.

XS
SM
MD
LG