Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:26

Obama apongeza juhudi za amani Ireland.


Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Ireland Enda Kenny.
Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Ireland Enda Kenny.

Rais Obama akutana na waziri mkuu wa Ireland na kupongeza juhudi zao za amani Ireland kaskazini.

Rais wa Marekani Barack Obama ameanza ziara huko Ireland kwa kupongeza juhudi zao za kuleta amani katika jimbo la Uingereza la Ireland kaskazini na kusema inatia moyo Marekani.

Baada ya kukutana na waziri mkuu wa Ireland Enda Kenny huko Dublin leo Bw. Obama amesema “maendeleo kuelekea amani Ireland kaskazini yanaonyesha kwa jinsi gani watu wanavyoweza kuangalia upya mahusiano yao katika mapambano ya muda mrefu”.

Rais pia alisema ziara ya kihistoria ya Malkia Elizabeth huko Ireland wiki iliyopita imewasaidia kuleta uhusiano mzuri baina ya pande zote mbili na inaleta “wimbi la matumaini” kwa mataifa mengine duniani.

Ziara ya Malikia Elizabeth ilikuwa ya kwanza kwa ufalme huo huko Ireland katika muda wa karne nzima.

XS
SM
MD
LG