Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:41

Obama aonya juu ya hatari za makundi yenye msimamo mkali Afrika


Rais wa Marekani Barack Obama amesema makundi ya wanamgambo yenye msimamo mkali yana mtizamo wa kuleta “ uharibifu na vifo “ kwa Afrika.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema mabomu huko Uganda ambayo yameuwa zaidi ya watu 70 waliokuwa wakiangalia fainali za kombe la dunia kwenye televisheni inaonyesha kuwa makundi ya wanamgambo yenye msimamo mkali yana mtizamo wa kuleta “ uharibifu na vifo “ kwa Afrika.

Katika mahojiano na shirika la Utangazaji la Afrika Kusini SABC , Bw.Obama alitofautisha mtazamo huu na ule wa Afrika ya kisasa iliyoungana.

Amesema pia mabomu haya ya kutisha yanaonyesha kuwa waislam wenye msimamo mkali waliodai kuhusika hawafikirii madhara ya muda mrefu wakati wakifanya vita vya kimawazo na kuuwa watu wasio na hatia.

Kundi la wanamgambo wa kisomali la Alshabab limedai kuhusika na mashambulizi hayo katika maeneo mawili ya mji mkuu wa Uganda Kampala. Kundi hilo lenye uhusiano na Al Qaida limesema mashambulizi hayo yalikuwa ni kulipiza kisasi kwa Uganda kushiriki kwenye jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika ambalo linaiunga mkono serikali ya Somalia na kwamba mashambulizi mengine yatafuatia.

XS
SM
MD
LG