Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:12

Obama alaani mashambulizi ya Garissa


Maafisa wakishuhudia watu waliouawa ndani ya kanisa baada ya mashambulizi mjini Garissa Julai 1
Maafisa wakishuhudia watu waliouawa ndani ya kanisa baada ya mashambulizi mjini Garissa Julai 1

Watu 17 waliuawa katika mashambulizi hayo, baadhi ya majeruhi wamefikishwa Nairobi kwa matibabu zaidi

Marekani imelaani vikali mashambulizi ya Jumapili katika makanisa mawili huko Garissa, Kenya na kuuwa watu wapatao 17 huku wengine zaidi ya 40 wakiwa wamejeruhiwa.

mashambulizi hayo ya Garissa yametokea siku chache kufuatia kuuawa kwa mfanyakazi mmoja wa misaada na kutekwa kwa wengine wanne kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab, na kabla ya hapo kulitokea shambulizi katika klabu moja ya starehe mjini Mombasa wiki iliyopita.

Taarifa ya White House iliyotolewa Washington Jumapili jioni ilisema watu waliofanya mashambulizi hayo hawakuonyesha heshima yoyote kwa maisha ya binadamu, na ni lazima wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria mapema iwezekanavyo.

XS
SM
MD
LG