Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:37

Obama: Afrika iwe muuzaji chakula nje


Rais Barack Obama ametoa changamoto kwa nchi za Afrika kufanya juhudi za kuwa wauzaji wakubwa wa chakula nje.

Rais Barack Obama wa Marekani amezitaka nchi za Afrika kufanya juhudi na kuwa wauzaji wakubwa wa chakula nje ya nchi kote duniani.

Akihutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York Alhamisi rais Obama alisema "hakuna sababu Afrika isiwe muuzaji mkubwa wa chakula nje." Aliongezea kuwa ndio sababu ameweka mipango nchini mwake ambaye itawezesha wakulima barani Afrika.

Alisema Marekani inafanya juhudi kuifanya dunia iwe wazi zaidi, na kuwezesha biashara na kuinua uchumi wa nchi zote duniani kwa ushirikiano katika nyanja zote. Alisema hakuna sababu kwa mfanyabiashara kulipa rushwa akitaka kufungua biashara, na kukumbusha kuwa wajibu wa serikali ni kuwezesha wananchi sio kuwabana.

XS
SM
MD
LG