Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:37

Obama afanya kampeni kwa ajili ya Clinton.


Rais Barack Obama katika picha
Rais Barack Obama katika picha

Obama atakuwa akihudhuria mkutano wa hadhara huko Philadelphia, ambako pia atahudhuria mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya chama cha democrat.

Rais Barack Obama wa Marekani anafanya kampeni leo Jumanne, kwa niaba ya waziri wake wa zamani wa wizara ya mambo ya nje Hillary Clinton, ambaye hivi sasa anapumzika kufuatia kuugua homa ya mapafu.

Obama atakuwa akihudhuria mkutano wa hadhara huko Philadelphia, ambako pia atahudhuria mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya chama cha democrat.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha CNN Jumatatu, Clinton alisema anategemea kurejea katika shughuli za kampeni baadaye wiki hii.

Wasaidizi wake wamesema wameghairi uamuzi wao wa kutoarifu umma kwamba Clinton alikuwa anaugua, kitu ambacho walifahamu Ijumaa, siku mbili kabla ya kuondoka ghafla kwenye shughuli ya maadhimisho ya mashambulizi ya kigaidi ya September 11 mjini New York .

Kuondoka kwake kulizua maswali kuhusu hali ya afya ya Bi Clinton.

XS
SM
MD
LG