Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 16:37

Obama: Lazima Marekani kuongoza tena duniani


Rais Barack Obama akitoa hotuba juu ya Hali ya Taifa bungeni, kati kati ya awamu ya madaraka yake.
Rais Barack Obama akitoa hotuba juu ya Hali ya Taifa bungeni, kati kati ya awamu ya madaraka yake.

Rais Barack Obama ametumia hotuba yake ya pili juu ya Hali ya Taifa kusisitiza juu ya malengo yake kwaajili ya taifa na kutoa wito wa uwekezaji katika kubuni, utafiti, maendeleo na miundo mbinu.

Marekani kuongoza duniani Obama

Katika hotuba yake Jumanne usiku kwenye baraza kuu la bunge, rais Obama alizungumzia jinsi ya kutanzua matatizo ya kiuchumi na kusema Marekani iko katika njia ya maendeleo. Lakini alisema nchi inabidi kufanya kazi kubwa zaidi kuhakikisha inabaki katika uwongozi na ushindanifu katika siku za mbele.

Alisema uwekezaji katika utafiti na elimu kutaweza kunufaisha sana Marekani, akitaja kwamba Urusi iliishinda Marekani kwenda angani 1957 kwa kurusha setaliti ya kwanza iliyojulikana kama Sputnik. Lakini baadae uwekezaji wa Marekani uliruhusu nchi hii kushinda katika mbiyo ya kufika mwezini.

Alisema uwekezaji huo ulipelekea wimbi kubwa la ubunifu na kujengwa viwanda vipya na mamilioni ya nafasi za ajira. Hivyo anasema kizazi cha sasa kiko katika kipindi cha "Sputnik"

Akizungumzia masuala ya kigeni, rais Obama alisema alisema Marekani imetekeleza miadi yake huko Irak na kwamba vita vinamalizika huko, huku ghasia zimepunguka, na serikali mpya imeundwa.

Rais wa Marekani alipongeza juhudi za wanajeshi na raia wa Marekani huko Afghanistan. Amesema dunia imebadilika katika miongo kadhaa ilyopita ambapo maduka madogo na makampuni yaMartekani yalikua yakinawiri yamefungwa, wafanyakazi wanapata mapato kidogo zaidi au kupoteza ajira zao.

China na India zinashindana sasa na biashara za Marekani. Kwa hivyo anasema hatua ya kwanza kupata ushindi wa siku za mbele ni kuhimiza uvumbiuzi wa Marekani, na inabidi kuchukua tena uwongozi duniani.

XS
SM
MD
LG