Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:44

Obama anaendelea kumfanyia kampeni Hillary


Rais Obama akiwasili North Las Vegas, kwenye kampeni. Oct. 23, 2016.
Rais Obama akiwasili North Las Vegas, kwenye kampeni. Oct. 23, 2016.

Rais wa Marekani Barack Obama alisema katika kinyang’anyiro cha kampeni za kuwania urais nchini Marekani kwamba mgombea wa Republican, Donald Trump, amejidhihirisha mwenyewe kwamba hafai kuwania madaraka ya kuingia White House.

Bwana Obama alimuunga mkono mwanachama mwenzake wa Democratic, Hillary Clinton anayewania urais katika uchaguzi wa Novemba nane wakati alipokuwa huko Las Vegas katika jimbo la Nevada akifanya kampeni kwa ajili ya Hillary siku ya Jumapili.

Obama aliendelea kusema kwamba Trump katika wiki za karibuni alirudia kulalamika kwamba utaratibu wa uchaguzi umeibwa dhidi yake kitu ambacho Rais Obama alisema kwamba inamaanisha Trump ameshindwa.

Wakati huo huo Clinton alikuwa na ujumbe sawa na huo kwenye kampeni zake huko Charlotte katika jibo la North Carolina akisema kwamba licha ya sera na kanuni tofauti za maraisi na wagombea wengi wa zamani hajawahi kuhoji kama walistahili kuongoza nchi au la.

XS
SM
MD
LG