Wamarekani na ulimwengu kwa ujumla wanaingojea kwa hamu hutoba ya Rais Barack Obama kuhusu hali ya Kitaifa hasa ikizingatiwa kuwa hii ndio hotuba ya mwisho ya aina yake ambayo Rais anaitoa akiwa madarakani.
Kuna matarajio mengi kwa wale wanaoishi Marekani na pia kwa ulimwengu kwani huu ndio mwaka wa uchaguzi mkuu wa Marekani na kwa hivyo wengi wanatarajia kuona kama atagusia swala hilo.
Swala la umiliki wa bunduki na pia usalama wa chi ni maswala muhimu yanayotarajiwa kuangaziwa bila kuacha nyuma janga la wahamiaji na hali ya uchumi. Kwenye mahojiano, Harrison Kamau wa VOA, amezungumza na Profesa David Monda kutoka jimbo la California na kumuuliza baadhi ya matarajio yake kabla ya hotuba hiyo kutolewa.