Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:04

Nyota wa kandanda duniani Maradona afariki


Mchezaji wa zamani maarufu Pele (kulia) akiwa na Diego Maradona wakati wa uhai wake Paris, France, June 9, 2016. REUTERS/Charles Platiau/File Photo
Mchezaji wa zamani maarufu Pele (kulia) akiwa na Diego Maradona wakati wa uhai wake Paris, France, June 9, 2016. REUTERS/Charles Platiau/File Photo

Mchezaji Hodari wa kandanda Diego Maradona, ambaye alikuwa anajulikana sana duniani kama mmoja wa wachezaji mahiri, amefariki kwa mshtuko wa moyo Jumatanbo, wakili wake amesema.

Maradona, alikuwa na umri wa miaka 60, hivi karibuni alikuwa na matatizo ya kiafya na kufanyiwa upasuaji baada ya damu kuganda kwenye ubongo wake wiki chache zilizopita.

Alipata mshtuko wa moyo akiwa nyumbani kwenye viunga vya mji mkuu wa Buenos Aires siku ya Jumantano nchini Argentina washirika wa karibu wa mchezaji huyo wa zamani walisema.

Rais wa Argentina, Alberto Fernandez ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Mchezaji mwingine maarufu wa kandanda kutoka Brazil, Pele alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanaomboleza kifo cha Maradona.

“Kwa kweli kuna siku, tutacheza mpira pamoja tukiwa mbinguni,” amesema Pele katika taarifa yake fupi kwa shirika la habari la Reuters.

Moja ya mambo ambayo Maradona atakumbukwa katika historia ya soka ni pale alipokuwa nahodha wa timu ya Argentina katika kombe la dunia mwaka 1986, kabla ya kuingia katika matatizo na kuondolewa katika kombe la dunia mwaka 1994, kwa kupima na kukutwa alikuwa ametumia dawa zilizopigwa marufuku.

Miaka kadhaa ya matumizi ya dawa, kula kupita kiasi na pombe viliingilia kati umahiri wake katika kandanda, mwaka 2000 alikaribia kupoteza maisha kwa kutumia dawa za kulevya.

XS
SM
MD
LG