Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 11:09

Argentina yaingia raundi ya pili, Nigeria nje


Marcos Rojo wa Argentina akifunga bao la ushindi dhidi ya Nigeria

Argentina ilihitaji goli la dakika za mwisho mwisho kuingia raundi ya pili ya fainali za kombe la dunia baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria. Kwa matokeo hayo Nigeria inarudi nyumbani na hivyo kuiwacha Senegal ikiwa timu pekee ya Afrika inayoweza kuingia raundi ya pili.

Argentina sasa itapamba na Ufaransa ambayo imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi C ikiwa na pointi saba baada ya kutoka sare 0-0 na Denmark katika mechi yao ya mwisho. Croatia itacheza na Denmark katika raundi ya pili baada ya kumaliza juu ya kundi D ikiwa na pointi tisa baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Iceland.

Lionel Messi baada ya kuipatia Argentina bao la kwanza
Lionel Messi baada ya kuipatia Argentina bao la kwanza

Ili kusonga mbele, Nigeria ilihitaji sare tu dhidi ya Argentina, na kwa muda mrefu ilionekana hali itakuwa hivyo baada ya Victor Moses kupata goli la kusawazisha kwa njia ya penalti katika dakika ya 51.

Lionel Messi alifungua mlango katika dakika ya 14 kwa goli safi ambalo liliipa Argentina nguvu kwa muda mrefu wa kipindi cha kwanza. Lakini Nigeria ilipata penalti muda mfupi tu baada ya kipindi cha pili kuanza.

Huku dakika zikiyoyoma ilionekana kuwa Nigeria watapata sare wanayohitaji kuingia raundi ya pili kwa jumla ya pointi nne. Lakini katika dakika ya 87 Marcos Rojo alifunga goli la ushindi kwa mkwaju mkali baada ya krosi kutoka upande wa kulia.

Jumatano kundi F linacheza mechi zake za mwisho huku timu tatu Mexico, Ujerumani na Sweden zikiwa na nafasi ya kuingia raundi ya pili. Ujerumani inapambana na Korea Kusini wakati Mexico inachuana na Sweden.

Kundi E pia linacheza mechi za mwisho Jumatano huku Brazil, Switzerland na Serbia zikiwa na uwezekano wa kuingia raundi ya pili. Brazil inapambana na Serbia wakati Switzerland inakumbana na Costa Rica ambayo tayari imetolewa katika mashindano baada ya kupoteza mechi zake mbili za kwanza.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG