Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:14

Nusu ya watu wa Haiti wanataabika na baa la njaa; inasemaWFP


Watoto wakiwa kwenye mstari wa kupokea chakula katika mji wa Port-au-Prince, Haiti. March 14, 2024.
Watoto wakiwa kwenye mstari wa kupokea chakula katika mji wa Port-au-Prince, Haiti. March 14, 2024.

Ongezeko la njaa linachochea mgogoro wa usalama unaoitikisa Haiti huku magenge ya uhalifu yakiendelea na harakati zake

Takribani nusu ya watu wa Haiti wanahangaika kujilisha, mashirika ya kimataifa yamesema Ijumaa, huku baadhi ya maeneo yakikaribia baa la njaa. Haiti sasa inakabiliwa na kiwango kibaya sana cha ukosefu wa chakula katika rekodi, kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani-WFP.

“Ongezeko la njaa linachochea mgogoro wa usalama ambao unaitikisa nchi. Tunahitaji hatua za haraka sasa, kusubiri kujibu kwa kiwango hicho sio chaguo”, alisema Jean-Martin Bauer, mkurugenzi wa Mpango wa Chakula Duniani kwa Haiti.

Wakati serikali ya mpito ya Haiti ikipambana kurejesha hali ya uthabiti, magenge yenye nguvu ya kisiwa hicho yameendelea kupiga hatua katika mji mkuu Port-au-Prince, afisa wa Umoja wa Mataifa amesema Alhamisi. Kuna uchovu mkubwa sana. Kuna mateso ya kibinadamu kwa kiwango cha kutisha.

Hofu kubwa. Kiwewe. Watu wamechoka tu”, Ulrika Richardson, mkazi wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Haiti, aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi katika mazungumzo kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

Katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, watu 2,500 waliuawa, kutekwa nyara au kujeruhiwa katika vurugu hizo, Richardson alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG