Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 20:55

NRM yapanga kumchukulia hatua za kinidhamu Amana Mbabazi


Waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi
Waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi

Chama tawala nchini Uganda cha NRM, kinapanga kumchukulia hatua za kinidhamu aliyekuwa Waziri Mkuu nchini humo, bwana Amama Mbabazi, hata baada ya kukosa kuchukua fomu za chama kuwania urais hatua inayomfanya Museveni kuwa mgombea pekee wa urais wa chama hicho.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:23 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Vyanzo ndani ya chama hicho vinaarifu kwamba viongozi wa chama wanapanga mikakati ya kumuondoa bwana Mbabazi ndani ya chama hata baada ya kukosa kuchukua fomu za chama kuwania urais hatua inayomfanya Rais Museveni kuwa mgombea pekee wa kiti cha urais wa chama hicho.

Lakini wakili wa bwana Mbabazi, bwana Freddy Mwema, alisisitiza kwamba ni uwamuzi wake binafsi bwana Mbabazi wa kuondoka ndani ya chama kwa hiyari au kwa kushurutishwa. “ni uwamuzi wake kuondoka ndani ya chama au la, kulingana na katiba ya chama hakuna anayeweza kumfukuza chamani na iwapo watamfukuza tutakabiliana nao kisheria”.

Mbabazi anaonekana kuwapa wakati mgumu viongozi wa chama cha NRM huku wakikosa kujua hatua yake itakayofuata huku akiamua kutozungumzia mipango yake iwapo atajiunga na vuguvugu la upinzani la Democratic Alliance na kuwania urais kupitia huko au ana mipango mingine ya kisiasa.

Makamu Rais wa zamani wa Uganda, Gilbert Bukenya
Makamu Rais wa zamani wa Uganda, Gilbert Bukenya

Wakati huo huo wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Uganda walimuunga mkono bwana Mbabazi kwa kutowania kiti cha urais kupitia chama cha NRM dhidi ya Rais Yoweri Museveni aliyeko madarakani kwa muda mrefu wakisema angefanya hivyo ni sawa na kupoteza muda.

Amana Mbabazi na Profesa Gilbert Bukenya ambaye alikuwa Makamu wa Rais nchini Uganda walitangaza kuwania kiti cha urais kupitia chama tawala.

XS
SM
MD
LG