Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 21:02

Novak Djokovic apata ushindi na kuingia robo fainali Australian Open


 Mserbia Novak Djokovic akishangilia ushinda mechi yake ya raundi ya nne dhidi ya Alex De Minaur wa Australia.REUTERS
Mserbia Novak Djokovic akishangilia ushinda mechi yake ya raundi ya nne dhidi ya Alex De Minaur wa Australia.REUTERS

Tennis mchezaji mkongwe Novak Djokovic alikata matumaini ya mchezaji Alex de Minaur kwa jumla ya seti 6-2, 6-1, 6-2  siku ya Jumatatu na kutinga robo fainali ya Australian Open .

Aliingia fainali hizo kwa ushindi huo katika harakati zake za kunyakua taji la 10 kwenye Grand Slam ambalo linatishiwa na tatizo la msuli wa paja.

Djokovic alifanya shambulio la kwanza baada ya kuanza kwa taabu kwenye mechi wakati De Minaur alipogonga mkono kwenye wavu na kuruhusu mchezaji huyo nambari nne kusonga mbele kwa pointi 4-2 na Mserbia huyo akaingia mapumziko na kushinda seti ya kwanza.

Akiwa hajawahi kupoteza mchezo Melbourne Park tangu raundi ya nne mwaka wa 2018, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, hakumpa nafasi De Minaur kwenye uwanja wa Rod Laver Arena, alipotoka nje ya eneo na kumtawala mpinzani wake kwa mikwaju ya mikali kwenye winga zote mbili.

Akiwa anaongoza kwa seti mbili kwa bila na huku msuli wake wa paja uliokuwa umefungwa bandeji kwa kiwasi kikubwa baada ya kuwa na wasi wasi katika raundi mbili zilizotangulia Djokovic aliingia kwa nguvu na kumaliza na kushinda michezo minne ya kwanza na kumaliza kwa staili akijiandaa kupambana na mchezaji nambari tano Andrey Rublev.

XS
SM
MD
LG