Awali mahakama kwa kauli moja ilitupilia mbali changamoto ya mchezaji huyo wa tenisi nambari 1 ya kufutwa kwa visa yake.
Djokovic, mwenye umri wa miaka 34 kutoka Serbia, alisema amesikitishwa sana na uamuzi huo lakini anauheshimu.
Mchezaji huyo akiwa amevaa barakoa alipigwa picha katika chumba cha mapumziko cha uwanja wa ndege wa Melbourne akiwa na maafisa wawili wa serikali waliovalia sare nyeusi. Aliondoka kwa ndege ya shirika la Emirates hadi Dubai, jiji lile lile la Umoja wa Falme za Kiarabu alikosafiri hadi Australia.
Djokovic ameshinda rekodi ya mataji tisa ya Australian Open, yakiwemo matatu mfululizo, lakini wakati huu hatapata nafasi ya kujaribu hilo.